Shirika la habari la Ahlubayt (as)ABNA: Edward Snowden aliyasema hayo jana baada ya kutolewa ripoti mpya kuhusu kashfa za ujasusi za programu ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya viongozi wa nchi mbalimbali, wanaharakani na waandishi wa habari.
Edward Snowden ameyasema hayo baada ya kampuni ya NSO inayotengeneza programu ya ujasusi ya Pegasus ambayo imebainika kuwa ilifanya ujasusi katika simu ya mkononi ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, kudai kuwa, haiwezekani kudukua simu za mkononi zinazoanza na kodi nambari ya +1.
Mfichuaji wa kashfa za kijasusi, Edward Snowden ambaye aliwahi kuwa mshauri wa Wakala wa Usalama wa Taifa nchini Marekani (NSA) amesema madai ya kampuni ya NSO kwamba haiwezekani kudukua nambari za simu zinazoanza na kodi ya simu za Marekani ni ya uongo mtupu.
Edward Snowden ambaye kwa sasa anaishi Russia, maiaka saba iliyopita alitoroka Marekani na kwenda Hong Kong ambako alifichua na kuanika maelfu ya nyaraka muhimu za kijasusi za serikali ya Marekani dhidi ya raia wa nchi hiyo; suala ambalo lilikuwa sawa na bomu la habari kote duniani.
Wakati huo huo afisa mmoja wa serikali ya Marekani ameliambia gazeti la Washington Post kwamba, ni ujinga kudhani kwamba, programu ya ujasusi ya Israel, NSO haiipatii serikali ya Tel Aviv data na taarifa nyeti za usalama wa taifa la Marekani.
Gazeti la Le Monde la Ufaransa limefichua kuwa, simu za mkononi za Rais Emmanuel Macron na viongozi wengine 15 wa serikali ya Ufaransa zimefanyiwa ujasusi na utawala wa Kizayuni kwa kutumia programu ya Pegasus.
Vilevile Uchunguzi uliofanywa kwa pamoja na mashirika ya habari ya Reuters, Washington Post, Wall Street Journal, al Jazeera na The Guardian unaonesha kuwa, shirika la kijasusi la NSO la Israel limetumia programu hiyo kufanya ujasusi mkubwa kote ulimwenguni.
342/